Kama ilivyotangazwa kwa makutaniko yote mwezi Juni 2026, tengenezo limeanzisha akaunti rasmi za mitandao ya kijamii za JW Pressroom kwenye Instagram na TikTok, katika lugha ya Kiingereza pekee.
JW Pressroom hutoa habari rasmi kwa umma kuhusu Mashahidi wa Yehova kwa watu kama vile maofisa wa serikali, waandishi wa habari, watafiti, na wengine wanaotafuta habari sahihi. Ingawa akaunti hizi za mitandao ya kijamii hazikukusudiwa hasa kwa ajili ya wahubiri, makala hii imetayarishwa hasa kwa ajili ya wahubiri ambao bado wanataka kuifuatilia akaunti hiyo.
Ikiwa wewe ni ofisa wa serikali, mwandishi wa habari, mtafiti, au mtu mwingine anayetafuta habari rasmi kuhusu Mashahidi wa Yehova, tafadhali endelea hapa ili kuwasiliana na Ofisi ya Habari za Umma ya Mashahidi wa Yehova.
Akaunti Rasmi
Jina rasmi la mtumiaji la JW Pressroom kwenye mitandao ya kijamii ni:
jw_pressroom
Jina hilo la mtumiaji limeundwa kwa herufi jw, zikifuatiwa na mstari wa chini mmoja (_), kisha neno pressroom. Linaweza pia kuonekana likiwa na alama ya @ kama hivi: @jw_pressroom
Iwe jukwaa linaonyesha jina hilo kama jw_pressroom au @jw_pressroom, tahajia yake lazima ilingane kabisa.
Kwa sasa, JW Pressroom inapatikana kwa Kiingereza pekee kwenye majukwaa yafuatayo:
Unaweza kubofya jina la kila jukwaa ili kufikia akaunti rasmi. Unaweza pia kutembelea jw.org® ili kuthibitisha akaunti rasmi za JW Pressroom kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa sasa JW Pressroom haipatikani kwenye jukwaa lingine lolote la mitandao ya kijamii wala katika lugha nyingine yoyote.
Unapochunguza akaunti hiyo, unaweza pia kuangalia kama kuna beji ya uthibitishaji au alama ya tiki ya uthibitishaji. Akaunti ya JW Pressroom kwenye Instagram kwa sasa inaonyesha beji ya uthibitishaji. Akaunti ya TikTok kwa sasa haionyeshi beji ya uthibitishaji, lakini inaweza kupata beji hiyo wakati ujao.
Hata hivyo, usitegemee mwonekano pekee. Kabla ya kuifuatilia akaunti hiyo au kushirikiana nayo, hakikisha jina la mtumiaji linalingana kabisa.